Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB Benki Bi. Tully Esther Mwambapa akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa Waziri  Mkuu Mh. Mizengo Pinda (MB), ili kusaidia huduma za Hospitali ya wilaya ya Bariadi baada ya ufunguzi wa tawi la Bariadi mkoani Shinyanga. Anayeshiriki kupokea hundi hiyo ni Mkuu wa mkoa Shinyanga Bw. Ali Nassoro Rufunga na wanaoshuhudia ni Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. John Cheyo (wakwanza kushoto) na Mbunge wa Bariadi Magharibi Mh. Andrew Chenge(wapili kushoto).